WAKALA wa Barabara nchini (Tanrods) na Kampuni ya ujenzi wa barabara ya M/S Strabag Internation GmbH ya Ujerumani, wamesaini mkataba wa ujenzi wa miundombinu ya usafiri wa mabasi yaendayo kasi kwa awamu ya kwanza wenye thamani ya Sh240.8 bilioni.
Mtendaji Mkuu wa Tanrods, Patrick Mfugale, alisema kwa mujibu wa mkataba huo, awamu hiyo ya kwanza itajumuisha ujenzi wa barabara ya Morogoro kutoka Kimara mpaka Kivukoni Feri, barabara ya Kawawa kutoka Magomeni hadi Morocco na kutoka Fire hadi barabara ya makutano ya Nyerere (Kamata).
Alisema kuwa ujenzi huo ambao unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 36 kuanzia sasa, utajumuisha vituo 29 vya kawaida vya mabasi hayo, vituo vikuu vitano, karakana mbili, ujenzi wa madaraja 3 ya watembea kwa miguu maeneo ya Ubungo, Kimara na Morocco.
Alisema mkataba wa ujenzi wa mfumo huo wa barabara wenye urefu wa kilomita 20.9 unatekelezwa kwa fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia (WB) ambayo imetoa Sh150 bilioni.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi jijini Dar es Salaam (DART) , Cosmas Takule, alisema mradi huo unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya watu kukataa kuhama katika maeneo wanayotakiwa kuhama kupisha miundombinu ya mradi huo.
“Kuna watu wengine wanataka kulipwa fidia kubwa kuliko ilivyopangwa na wanafungua kesi mahakamani hali inayochelewesha mradi,” alisema Takule.
Waziri wa Ujenzi , Dk John Magufuli ambaye alishuhudia utiwaji saini wa mkataba huo, alimtaka mkandarasi anayejenga miundombinu hiyo, kuhakikisha anakamilisha ujenzi kwa wakati na ikibidi iwe kabla ya muda waliokubaliana.
“Dar es Salaam kuna msongamano mkubwa sana wa magari, ikibidi hakikisheni mnamaliza kazi kabla ya muda tuliokubaliana,” alisema Dk Magufuli.Aliwataka pia watu wanaotakiwa kupisha ujenzi huo, kufanya hivyo haraka kwa kuwa wanachelewesha kumalizika kwa tatizo la foleni.

No comments:
Post a Comment