Friday, May 25, 2012

Mgosi aiombea msaada familia ya Mafisango


Mussa Mgosi.
Na Khatimu Naheka
KIUNGO mshambuliaji wa DC Motema Pembe ya DR Congo, Mussa Mgosi, amezitaka klabu za Simba na Azam FC kufikiria juu ya kuisaidia familia ya kiungo wa zamani wa timu hizo, Patrick Mafisango.
Mafisango ambaye alifariki Alhamisi iliyopita aliwahi kuzichezea klabu hizo kwa nyakati tofauti, ambapo katika msimu uliomalizika alikuwa msaada mkubwa katika kuipa Simba ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kufunga mabao 11 kwenye ligi hiyo.
Akizungumza kutoka mjini Kinshasa, Mgosi aliyewahi kucheza na Mafisango akiwa Simba kabla ya kutimkia DC Motema Pembe amesema kifo cha mchezaji huyo kimeacha hali ngumu kwenye familia yake.
Alisema marehemu ameacha watoto watatu ambao anaamini wanaweza kuwa na wakati mgumu kutokana na hali ya maisha ya DR Congo.
“Huku (DR Congo) maisha ni magumu sana, marehemu ndiye alikuwa kila kitu katika familia yake sasa kifo chake kimefanya familia yake kuwa kwenye hali tata, natoa wito kwa Simba na Azam kuangalia uwezekano wa kuisaidia hii familia kwa chochote,” alisema Mgosi.

g


Jack Dustan ‘Jack Maisha Plus’.
Na Erick, Evarist
MSANII wa Filamu, Jack Dustan ‘Jack Maisha Plus’ hivi karibuni alinaswa akiwa amevalia nusu uchi huku akiwa bwii kwa pombe.
Tukio hilo la aibu lilinaswa na paparazi wetu ndani ya Ukumbi wa Business Park uliopo Makumbusho jijini Dar ambapo Bendi ya Mashujaa ilikuwa ikiporomosha burudani.
Awali, mrembo huyo alionekana akizama ukumbini hapo akiwa ameongozana na msanii mwenzake, Husna Idd ‘Sajent’ huku akiwa amevaa kigauni kilichoacha mapaja yake wazi.
Moja kwa mjoa walikwenda kuketi kwenye meza iliyokuwa pembeni kisha kuanza kuagiza pombe kwa fujo ambapo ndani ya muda mfupi, al ionekana akiwa tillila hivyo kufanya vituko vya hapa na pale.

NAIBU WAZIRI JANUARY MAKAMBA ATEMBELEA AIRTEL

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (kushoto) akipokewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sam Elangallor, alipofanya ziara kukagua shughuli mbalimbali za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasilino wa Airtel, Beatrice Singano Mallya.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (kushoto) akipokewa na Ofisa Mkuu wa Biashara wa Airtel Tanzania, Chiruwi Walingo alipokwenda kufanya ziara ili kukagua shughuli mbalimbali za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya akiongozana na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (kushoto) katika ofisi za makao makuu ya Airtel wakati wa ziara yake kukagua shughuli mbalimbali za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sam Elangallor (katikati) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (kulia) na ujumbe wake wakati wa ziara ya naibu waziri huyo kukagua shughuli mbalimbali za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.



STEVE NYERERE ATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA, AZINDUA FILAMU YAKE KINONDONI JIJINI DAR


Msanii Steven Mangele 'Steve Nyerere' (katikati) akiwa na Ofisa wa Kampuni ya Steps, Pritesh Chavda (kulia) na Mwandishi wa Habari wa Kituo cha EATV, Patrick Nyembela wakati alipokwenda kutembelea Kituo cha Watoto Yatima cha Maunga kilichopo Kinondoni na kutoa misaada ya vyakula mbalimbali kwa ajili ya uzinduzi wake wa filamu ya 'Nyerere' jana.
Steven Mengele 'Steve Nyerere' (kushoto) akimkabidhi chandarua mtoto Ally Hussein wakati alipokwenda kutoa misaada mbalimbali na kufanya utambulisho wa filamu yake mpya ya Nyerere jana.…


Msanii Steven Mangele 'Steve Nyerere' (katikati) akiwa na Ofisa wa Kampuni ya Steps, Pritesh Chavda (kulia) na Mwandishi wa Habari wa Kituo cha EATV, Patrick Nyembela wakati alipokwenda kutembelea Kituo cha Watoto Yatima cha Maunga kilichopo Kinondoni na kutoa misaada ya vyakula mbalimbali kwa ajili ya uzinduzi wake wa filamu ya 'Nyerere' jana.
Steven Mengele 'Steve Nyerere' (kushoto) akimkabidhi chandarua mtoto Ally Hussein wakati alipokwenda kutoa misaada mbalimbali na kufanya utambulisho wa filamu yake mpya ya Nyerere jana.

Steve akikabidhi maharage kwa mama mlezi wa kituo cha Maunga kilichopo Kinondoni Dar es Salaam, Bi. Zainabu Bakari alipokwenda kutoa misaada ya vyakula na vitu mbalimbali.
Steven Mengele 'Steve Nyerere'  (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Maunga Kinondoni jijini Dar es Salaam.
'Steve Nyerere' akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa kutambulisha filamu yake ya Nyerere.

Msemaji wa Kampuni ya Steps ya jijini Dar es Salaam, Kambarage Ignatios (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wa uzinduzi wa filamu ya Nyerere.
Mkurugenzi wa DJ Marketing and Promotion, Daniel Haule akibandika bango la filamu mpya ya Nyerere iliyozinduliwa jana.
Mkurugenzi wa DJ Marketing and Promotion, Daniel Haule (kushoto) na Msemaji wa Kampuni ya Steps ya jijini Dar es Salaam, Kambarage Ignatios wakibandika bango la filamu mpya ya Nyerere iliyozinduliwa jana.



Wema Sepetu na Jacob Steven ‘JB’ wakiwa katika pozi.

Wema na JB wakiingia hotelini.
Na Imelda Mtema
MASTAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu na Jacob Steven ‘JB’ hivi karibuni walizua jambo walipokuwa Zanzibar kufuatia mapozi tata waliyokuwa wakijiachia nayo mbele za watu.
JB na Wema ambao walikuwa miongoni mwa wasanii waliokwenda kumpa ‘tafu’ mwenzao, Issa Musa ‘Claud’ kwenye uzinduzi wa filamu yake ya Toba uliofanyika ndani ya Hoteli ya Bwawani, walionekana wamegandana kiasi cha baadhi ya watu kudhani ni Mr na Mrs.
Awali, wawili hao walizama hotelini hapo huku JB akiwa amemuweka ‘kwapani’ Wema lakini hata walipoingia ndani, walikaa pamoja.
Aidha, tukio lililozidisha minong’ono ni lile la Wema kuegamia mabegani mwa JB kisha kuuchapa
ambapo mmoja wa watu waliokuwepo ukumbuni hapo alisikika akisema: “Mh...wana mambo hawa, atawezaje kumlalia mwanaume ambaye siyo wake hadi kulala vilee?”


DIAMOND ACHAFUKA UKWENI



Diamond akiwa amemkumbatia na Wema.

...Akiwa amemwinamia na Aunt Ezekiel.…


Diamond akiwa amemkumbatia na Wema.

...Akiwa amemwinamia na Aunt Ezekiel.
Naseeb Abdul ‘Diamond’.
Jokate Mwegelo.
Na Shakoor Jongo
ILE skendo ya kunaswa hotelini na mcheza sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel bado inamtesa mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’ ambapo safari hii anadaiwa kuchafuka vibaya upande wa wakwe zake kwa mchumba’ke Jokate Mwegelo, Ijumaa linafunguka.
Habari kutoka kwenye chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa wawili hao zinadai kuwa baada ya habari hiyo kubumburuliwa na gazeti damu moja na hili, Risasi Jumamosi ndiyo iliyotibua mambo ukweni kwake hivyo kuonekana siyo.
MSURURU WA WANAWAKE
Ilidaiwa kuwa habari hiyo ndiyo iliyotonesha kidonda kilichokuwa kinataka kukauka cha ‘kichaa’ huyo wa Bongo Fleva kutajwa kutoka kimapenzi na msururu wa wanawake mastaa na wasiokuwa mastaa.
“Asikwambie mtu, unajua upande wa akina Jokate ni watu wa dini sana. Yaani kwa skendo skendo kama hizo, wanamuona Diamond kama anataka kuwachafua.
“Unajua zile ishu za kudaiwa kutoka kimapenzi na msururu wa wanawake zilikuwa zimeanza kutulia kwa sababu yupo na Jokate lakini baada ya kutokea hii ya kunaswa hotelini na Aunt, imetibua mambo kule ukweni na mbaya zaidi anaonekana hajatulia,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutochorwa jina gazetini.
HUYU HAPA DIAMOND
Ili kupata mzani wa habari hiyo, Ijumaa lilimvaa Diamond kavukavu ambapo katika kuthibitisha kuwa vyanzo vyetu vya habari havibahatishi, alikiri kuchafuka ukweni huku akiongeza kuwa anahisi kuna watu nyuma ya habari hizo ambao wamelenga kumharibia mambo yake.
“Naomba niweke wazi jambo hili kwa sababu ni kweli nachafuliwa.
“Kuna watu wananichafua ili nionekane kituko kwenye familia ya akina Jokate, nahisi wanaweza kufanikiwa,” alisema Diamond Platnumz.
UHUSIANO WAKE NA JOKATE
Kufuatia ishu hizo, uhusiano wa kimapenzi wa kidume huyo na mwanamitindo Jokate unadaiwa kuwa kwenye hatihati pamoja na kwamba bado wapo pamoja.
TULIKOTOKA
Mwishoni mwa wiki iliyopita Diamond na Aunt walidaiwa kubambwa katika Hoteli ya Kebby’s iliyopo Mwenge, Dar wakila ‘good time’, hivyo kuzua tafrani kwenye uchumba wa mwanamuzi huyo na Jokate.
Mbali na madai hayo yanayomhusisha Diamond na Aunt ‘kuminya’ pamoja, kichwa hicho cha Bongo Fleva kiliwahi pia kutajwa kutoka na mwigizaji Jacqueline Wolper, wauza nyago kwenye video za muziki, Rehema Fabian na Natasha, staa wa Maisha Plus, Pendo Moshi kabla ya kumchumbia Wema Sepetu kisha wakamwagana na kujikuta mikononi mwa Jokate.