UKURASA wa kwanza wa gazeti hili tumechapisha habari ya Rais Jakaya Kikwete akiwataka wakazi wanaoishi mabondeni kuhama ili kuondokana kukumbwa na maafa mengine yanayoweza kutokea katika siku zitajazo.
Rais Kikwete alisema inasikitisha kuona wakati Watanzania tunaomba usiku na mchana mvua inyeshe ili mazao yastawi, wapo wenzetu ambao wanaomba jua liwake mwaka mzima ili waendelee kuishi maeneo yasiyoruhusiwa ya mabondeni.Vilevile, Serikali imesema kwamba itatenga eneo la wakazi waishio mabondeni waweze kuhamia.
Agizo la Rais Kikwete linafuatia mvua kubwa iliyonyesha jijini Dar es Salaam kwa siku tatu mfululizo kuanzia Desemba 20 mwaka huu, na kusababisha vifo vya watu 30 na majeruhi 50.
Tunachukua nafasi hii kumpongeza Rais Kikwete kwa kuchukua uamuzi huu ambao utasaidia kunusuru maisha ya mamia ya watu ambao wanaishi katika maeneo hayo jijini Dar es Salaam.
Kutokana na wananchi kupoteza maisha, mali na miundombinu mingi kuharibika hili ni janga la kitaifa na kama tulivyosema katika tahariri yetu ya gazeti la jana kuwa Serikali ihakikishe inawahudumia wananchi wote walioathirika na mafuriko haya.
Pamoja na Serikali kutenga eneo la kuwahamishia wakazi, ikiwa ni pamoja na kuwapatia misaada wale wote waliokumbana na mafuriko hayo ambapo nyumba zao zilianguka na kisha kusombwa na maji,
lakini sisi tunasisitiza kwamba agizo la Rais Kikwete kuwataka wananchi wanaoishi mabondeni kuhama lisimamiwe na kutekelezwa watendaji wa Serikali.
Hii sio mara ya kwanza kwa viongozi wa Serikali kuwataka wananchi wanaoishi katika maeneo ya mabondeni jijini Dar es Salaam kuhama mara mvua kubwa zinaponyesha na kuleta madhara.
Tunakumbuka vyema Serikali iliwahi kulitangaza eneo la Jangwani kuwa ni eneo la maafa na hivyo kuwataka wakazi wote wa eneo hilo kuhama, lakini, hakuna mtu ambaye alihama.
Kama hiyo haitoshi, Serikali iliwahi kuwavunjia nyumba wakazi wa eneo la Jangwani kuwalazimisha kuhama, lakini zoezi hili lilisitishwa baada ya wakazi wa eneo hilo kukimbilia kwa viongozi chama tawala na baadaye wakakingiwa kifua kuwa ni wapigakura wasibughudhiwe.
Kutokana na uzoefu huo, tunadhani sasa maafa haya yaliyotokea wiki hii, agizo la Rais litekelezwe kwa vitendo na mtendaji wa Serikali ambaye atashindwa kulisimamia awajibishwe.
Tutakuwa ni nchi pekee duniani ambayo wananchi wake wanaweza kuvunja sheria watakavyo, huku Serikali ambayo inatakiwa kuwawajibisha ikiwachekea na pengine kuwakingia kifua kwa kisingizio kuwa eti ni wapigakura.
Ili kuondokana na hali hii ya wananchi kuvamia maeneo ya mabondeni, ni vyema Serikali itunge sheria mpya ya ujenzi na kuweka viwango vya ujenzi vyenye hadhi ya kimataifa na hasa ujenzi wa kuta mbalimbali,majengo marefu ili kuhakikisha ujenzi holela haujitokezi kwenye miji na majiji.
Alama za nguzo kubwa ziwekwe katika mipaka ya maeneo ya makazi na mabonde ili maeneo hayo yabakie wazi.
Kitengo cha maafa kilichopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu nacho kinatakiwa kuimarishwa ili kiwe na uwezo wa kukabiliana na maafa yanapotokea.
Inavyoonekana kitengo hiki hakijaandaliwa vizuri kutokana na kushindwa kukabiliana na majukumu yanavyopaswa kufanywa wakati wa matatizo makubwa ya maafa.
Katika janga hili la mafuriko, inasikitisha kuona kwamba hata vifaa ya kujiokoa kwenye maji, Serikali haina hadi kufikia mahali Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadick atafute Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na mamlaka nyingine. Ni maoni yangu kwamba zoezi la kuwahamisha wakazi waishio mabondeni litafanywa kwa umakini ikiwa ni pamoja kuwapa msaada ya ujenzi watu hawa ambao wengi wao hawana kipato.

No comments:
Post a Comment