Friday, May 25, 2012

STEVE NYERERE ATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA, AZINDUA FILAMU YAKE KINONDONI JIJINI DAR

Msanii Steven Mangele 'Steve Nyerere' (katikati) akiwa na Ofisa wa Kampuni ya Steps, Pritesh Chavda (kulia) na Mwandishi wa Habari wa Kituo cha EATV, Patrick Nyembela wakati alipokwenda kutembelea Kituo cha Watoto Yatima cha Maunga kilichopo Kinondoni na kutoa misaada ya vyakula mbalimbali kwa ajili ya uzinduzi wake wa filamu ya 'Nyerere' jana.
Steven Mengele 'Steve Nyerere' (kushoto) akimkabidhi chandarua mtoto Ally Hussein wakati alipokwenda kutoa misaada mbalimbali na kufanya utambulisho wa filamu yake mpya ya Nyerere jana.…

Msanii Steven Mangele 'Steve Nyerere' (katikati) akiwa na Ofisa wa Kampuni ya Steps, Pritesh Chavda (kulia) na Mwandishi wa Habari wa Kituo cha EATV, Patrick Nyembela wakati alipokwenda kutembelea Kituo cha Watoto Yatima cha Maunga kilichopo Kinondoni na kutoa misaada ya vyakula mbalimbali kwa ajili ya uzinduzi wake wa filamu ya 'Nyerere' jana.
Steven Mengele 'Steve Nyerere' (kushoto) akimkabidhi chandarua mtoto Ally Hussein wakati alipokwenda kutoa misaada mbalimbali na kufanya utambulisho wa filamu yake mpya ya Nyerere jana.

Steve akikabidhi maharage kwa mama mlezi wa kituo cha Maunga kilichopo Kinondoni Dar es Salaam, Bi. Zainabu Bakari alipokwenda kutoa misaada ya vyakula na vitu mbalimbali.
Steven Mengele 'Steve Nyerere'  (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Maunga Kinondoni jijini Dar es Salaam.
'Steve Nyerere' akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa kutambulisha filamu yake ya Nyerere.

Msemaji wa Kampuni ya Steps ya jijini Dar es Salaam, Kambarage Ignatios (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wa uzinduzi wa filamu ya Nyerere.
Mkurugenzi wa DJ Marketing and Promotion, Daniel Haule akibandika bango la filamu mpya ya Nyerere iliyozinduliwa jana.
Mkurugenzi wa DJ Marketing and Promotion, Daniel Haule (kushoto) na Msemaji wa Kampuni ya Steps ya jijini Dar es Salaam, Kambarage Ignatios wakibandika bango la filamu mpya ya Nyerere iliyozinduliwa jana.

No comments:

Post a Comment